25 Novemba 2019 - 07:25
Watu laki tano wanahitaji misaada huko Sudan

Viongozi wa Sudan wametangaza kuwa watu laki tano wanahitaji misaada mbalimbali ya kibinadamu kutokana na mafuriko makubwa yaliyoiathiri nchi hiyo hivi karibuni.

(ABNA24.com) Abola John Naibu Gavana wa mkoa wa Boma kusini mashariki mwa Sudan ametangaza kuwa watu 70 wengi wao wakiwa ni watoto na wazee wamepoteza maisha tangu mwezi Oktoba mwaka huu kufuatia kujiri mafuriko hayo makubwa.

Ripoti nyingine kutoka mkoani humo zinaarifu kuwa karibu watu laki tano wanahitaji pia misaada mbalimbali ya kibinadamu. Sudan inaendelea kukumbuwa na athari za mvua zilizonyesha mwanzoni mwa mwezi Agosti.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa mafuriko hayo yameathiri maisha ya watu  245,700 na mbali na kubomoa nyumba elfu 32 na 851 yameharibu pia nyumba nyingine 284. 

.........
340